• USIHOFU JUU YA MAMBO YA DUNIANI KUWA NA HOFU ya MUNGU

  • Aug 13 2021
  • Duración: 15 m
  • Podcast

USIHOFU JUU YA MAMBO YA DUNIANI KUWA NA HOFU ya MUNGU  Por  arte de portada

USIHOFU JUU YA MAMBO YA DUNIANI KUWA NA HOFU ya MUNGU

  • Resumen

  • 1 Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu.
    Ufunuo wa Yohana 2:1

    2 Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo;
    Ufunuo wa Yohana 2:2

    3 tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka.
    Ufunuo wa Yohana 2:3

    4 Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza.
    Ufunuo wa Yohana 2:4

    5 Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.
    Ufunuo wa Yohana 2:5

    6 Lakini unalo neno hili, kwamba wayachukia matendo ya Wanikolai, ambayo na mimi nayachukia.
    Ufunuo wa Yohana 2:6

    7 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.
    Ufunuo wa Yohana 2:7

    8 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika; Haya ndiyo aneneyo yeye aliye wa kwanza na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai.
    Ufunuo wa Yohana 2:8

    9 Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani.
    Ufunuo wa Yohana 2:9

    10 Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.
    Ufunuo wa Yohana 2:10

    11 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.
    Ufunuo wa Yohana 2:11

    12 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili.
    Ufunuo wa Yohana 2:12

    13 Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.
    Ufunuo wa Yohana 2:13
    Más Menos
activate_primeday_promo_in_buybox_DT

Lo que los oyentes dicen sobre USIHOFU JUU YA MAMBO YA DUNIANI KUWA NA HOFU ya MUNGU

Calificaciones medias de los clientes

Reseñas - Selecciona las pestañas a continuación para cambiar el origen de las reseñas.