Salama Na  By  cover art

Salama Na

By: Salama Na
  • Summary

  • ‘Salama na’ – meaning ‘Salama and’ is a one hour Podcast chat show hosted by a re known Radio &; TV personality Salama Jabir and available on Both Video and Audio of Various Platforms. In Salama na, Salama gets to sit down for exclusive chats with Celebrities, Influencers and Change makers in the society. Support this podcast: https://podcasters.spotify.com/pod/show/yahstonetown/support
    Salama Na
    Show more Show less
Episodes
  • SE7EP38 - SALAMA NA MFAUMEX2 | TOE - TO - TOE
    Mar 2 2023

    Mfaume Mfaume ni yule mwana ambaye akitokea sehemu ni sahihi kwako kuwaambia wahusika kwamba jamani, mwamba huyu hapa! Muonekano wake pekee unamfanya mtu ajue yuko kwenye presence na mtu maalum na baadae ukishajua hasa nini anafanya basi huwezi ku doubt yote ambayo utaambiwa juu yake lakini kubwa zaidi ukipata sasa nafasi ya kumuona anapokua kazini kwake hapo ndo utakaposhia kumpa nyota zake zote anazostahili kama bondia. Tena popote pale, iwe akiwa gym au ulingoni ambapo kadhaa washachezea shurba kutoka kwake.

    Mfaume ni kama wengi wetu ambao tumetokea katika familia za kawaida tu ambayo malengo ya wazazi wetu kwetu ni kuhakikisha unasoma ili uweze kupata kazi nzuri na uje uwasaidie wao na Ndugu zako utakapokua mkubwa, vile vile mambo ya michezo ni kawaida maana kama mtoto unapokua unakua shuleni na mtaani ni lazima kunakua na kucheza, chochote ambacho kiko mbele lakini zaidi huwa ni mpira wa miguu kwa Kaka zetu ingawa sasa dunia imebadilika kiasi, siku hizi hata watoto wa kike kucheza soka ni jambo la kawaida tu na kwa hilo napenda sana.

    So kwa Mfaume ni kama kwetu wengine tu, alianza kwa kucheza mpira lakini baadae interest yake ikatoka kutoka kwenye mpira na kuhamia kwenye ngumi, kwa wazazi wake huo ulikua mitihani hasa. Kwa mzazi kukuona mtoto wake akichezea vitasa mara kwa mara haliwezi kuwa jambo la kupokelewa kwa mikono miwili ndani ya nyumba, mtoto anarudi nyumbani kutoka kujifua nae anakua kafuliwa kwelikweli au akijua kwamba una pambano na mwamba flani aliye shindikana ndo hofu inapanda mpaka juu ya dari na inaeleweka kwanini inakua hivyo na kama mpaka sasa hujaelewa au hujaipatia picha basi mwenzetu huna moyo lol.

    Alinipa story moja kwenye maogezi yetu haya kuhusu Mama yake, ananiambia kuna wakati alikua na mechi na bondia ambaye alikua anaongea sana, anajisifia na kumtishia sana maisha yake, kwamba atamchakaza vibaya sana tena mbele ya Mama yake, na aliyasema hayo akijua fika Mfaume huwa anaenda na Bi Mkubwa wake kwenye fight zake zote za ndani, ananiambia Mama yake aliogopa sana, alimsihi sana lakini kwa jitihada zake na maguvu ya Allah aliweza kumaliza mchezo wake huo vizuri tu.

    Mabondia ni watu ambao wana roho za kipekee sana, unaweza ukamkuta mtu akiwa uliongoni anatoa dozi nzito kwa mpinzani wake ukadhani ni mtu mwenye roho mbaya sana, lakini ukimkuta nje ya ulingo na kwa watu wake utajua ni mtu wa aina nyengine kabisa. Kwa bahati nzuri nna marafiki ambao wanacheza mchezo huu wa boxing ikiwa pamoja na Mfaume mwenyewe, huwa ni watu wakarimu sana na wana mapenzi ya kweli lakini akiwa uliongoni anakua mtu mwengine kabisa, nadhani hiyo ndo tofauti ya masumbwi na michezo mengine.

    Yangu matumaini uta enjoy session yetu hii ya mwisho ya msimu huu na mwana huyo humble kutoka kitaa, na pia kama kawaida utaokota mawili matatu ambayo yatakusogeza sehemu.

    Tafadhali enjoy.

    Love,

    Salama.

    --- Support this podcast: https://podcasters.spotify.com/pod/show/yahstonetown/support
    Show more Show less
    1 hr
  • SE7EP37 - SALAMA NA TOUFIQ | Um'PENDAE
    Feb 23 2023

    Toufiq ni moja ya majina makubwa kati ya wafanya biashara wazuri na sasa mwanasiasa na Mbunge wa Mpendae, kwa wazee na vijana wa visiwani humo yeye ni mmoja wa mifano ya kuigwa ingawa kwake yeye yaliyo mengi kwenye maisha yake ni nguvu kubwa ilifanywa na Marehemu Mzee wake Ndugu Salih Hassan Abdullah Turky aka Mr White ambaye na yeye akiacha ukweli kwamba alikua tajiri na mfanya biashara nzuri huko visiwani ila yeye pia alikua kipenzi cha wananchi wa Jimbo la Mpendae ambapo sasa Toufiq ndo anaye liongoza jimbo hilo baada ya Mzee wake kutangulia mbele ya haki. Mwenyezi Mungu Amrehemu.


    Kwenye meza yetu ya kigae na kiti chetu kikukuu Taufiq anakumbuka wakati wa msiba wa Mzee wake bado wa moto kabisa watu walikua wanakuja nyumbani kwao na kumshauri yeye agombee ubunge wa jimbo hilo ambalo Mzee wake alikua akiliongoza. Ikumbukwe Mzee wake Mr White alifariki kipindi ambacho wananchi walikua wanajiandaa kwa uchaguzi wa wabunge wawakilishi na Rais, ananiambia kwanza aliwafukuza watu hao, wakarudi tena baada ya maziko bado Toufiq akawakatalia, baadae baada ya mambo kutulizana na kuombeleza kupungua watu ambao anawaheshimu walimfuata tena na kumueleza umuhimu wa yeye kugombea jimbo hilo. Wakamuelezea umuhimu wa Marehemu Mzee wake kwa watu wa Mpendae na kwamba kama hatofanya hivyo basi haitakua jambo zuri kwa wakazi wa eneo hilo. Ndugu Turky ilibidi akubaliane na ombi hilo na kutimiza matakwa ya wana Mpendae ambao walimpa kura nyingi za ndio.


    Yeye mawazo yake yalikua kwenye kuendeleza biashara zaidi ambayo kwa kiasi kikubwa Mzee wake alikua alimshirikisha nayo toka akiwa mdogo. Kuweza kufanya yote hayo kwa kijana mdogo kama yeye pengine ingekua mambo mengi sana so kwa heshima wakati mambo mengine yanaenda Toufiq ilibidi aachie majukumu mengine kwa Mdogo wake wa Kiume Ndugu Abdallah Salim na Dada yake Bi Khaytham Salim Turky, ingawa bado yeye ndo Mwenyekiti wa makampuni hayo ambayo yamejikita katika biashara mbali mbali ambazo zimestawi visiwani Zanzibar na nchi nyengine.


    Toufiq alikuja kwenye maongezi haya akiwa na mambo yake mengine ya ki majukumu kwenye meza yake na ki ukweli hatukupata wasaa teeele wa kuweza kuyachambua mengi kama ambavyo tungependa lakini pia hatukukosa lolote jambo la lolote jambo hilo ndo tumaini letu litasaidia kwenye kukusogeza kwenye sehemu fulani katika uelewa na uchambuzi wako wa mambo.

    Tafadhali enjoy hiki kidogo ambacho tuliweza kukukusanyia kwenye muda mchache.


    Love,

    Salama.

    --- Support this podcast: https://podcasters.spotify.com/pod/show/yahstonetown/support
    Show more Show less
    36 mins
  • SE7EP36 - SALAMA NA ALLY BEE | KULE NI KULE…
    Feb 16 2023

    Kwenye jiji la ‘Maraha’ hapa nyumbani kwetu Tanzania ambayo kwa miaka ya hivi karibuni sehemu za starehe zimekua tele na kila mmoja ana uwezo wa kula bata zake vizuri tu kulingana na urefu wa mfuko wake basi hakuna ambaye HAJUI jina la DJ huyu mahiri ambaye kwa ubunifu wake ameweza sana kubadilisha kabisa jinsi ambavyo wenzake walomtangulia walikua wanafanya. Yaani Ally alikichukua kitabu cha jinsi ya kutoa burudani kama DJ na kukichanachana na kisha akaanza kuandika cha kwake, ambacho mpaka tunaenda mtamboni kiiila msomaji wake anapeeenda ambayo yameandikwa na ambayo anaendelea kuyaandika.

    Wakati msimu huu unaanza Ally Bee hakua moja ya majina ambayo yalikua yameandikwa kama mmoja ya watu ambao tungependa kujua story ya maisha yake, kutaka kujua nini kinampa hamasa ya kufanya ambacho anafanya na pengine mambo mengine tele ambayo atakua na uhuru wa ku share na sisi. Ila kuna siku nilikua nyumbani na Rafiki yangu ambaye pia ni mdogo wangu Ndugu Sadam Almando Sanare ambaye nilikua namuuliza maswali kuhusu Dj mwengine kabisa huku nikilalamika kuhusu huyo mtu kwamba pengine kuna jambo haliko sawa kuhusu simulizi zake za baadhi ya mambo maana amekua kama anaongelea sana skuizi, then yeye akaniambia kuhusu Ally Bee (binafsi hupenda kumuita Ally Bee kwasababu wote tunamjua nyuki, na ukali wake lakini asali yake sote ndo kama hivyo, hopefully it will make sense kwake someday 😄). So wakati ananiambia nami tayari nilikua nishamuona, basi mengine yakaendelea kwenye meza yetu adhimu.

    Story ya maisha yake Ndugu yetu huyu ni ya mateso mengi sana, ila kwa sasa na hata pengine mwanzo kwa adha zote hizo tunamshukuru Allah kwa hayo yote maana hayo ndo yameleta hasira za yeye kutaka zaidi, kuomba zaidi na kufanyia kazi zaidi yote ambayo anayo leo. Ally anakumbuka jinsi alivyofika Dar es Salaam mara ya kwanza na pia amenihadithia adha ya kutokua na sehemu ya kukaa hasa unapokua umekuja mjini mara ya kwanza. Alinifanya nijiulize maswali mengi sana mimi kama binadamu wa kawaida kabisa, au ambaye Mwenyezi kanibariki kwa mengi zaidi ya wengine, nini nafanya kuwasaidia ambao nawaona barabarani? Au ambao hawana uwezo wa kunifikia lakini wana uhitaji? Kanifundisha kuhusu kutochukulia maisha au nafasi ambazo tunazo kwenye maisha yetu kwamba ni kawaida tu. Ki ukweli kila ambacho tunacho kwenye maisha yetu TUNA KILA SABABU YA KUMSHUKURU AMBAYE AMETUPA. Ila pia inabidi mara moja moja tujipigie makofi kwa mbali ambapo tumetoka na ambapo tumefika lakini zaidi tumuombe Mwenyezi Mungu azidi kutuimarisha na kutufungulia milango ya Kheri, ZAIDI.

    Niamini mimi nikikuambia kuhusu kutoa, kwamba kutoa ni raha zaidi kuliko kupokea ingawa wengi wetu tunapenda zaidi kupokea, ukitaka kujua hilo jaribu kwa kuanza kumpa hata mtu zawadi ndogo tu, hata pipi ambayo alikua hategemei kama utampa au utakumbuka, sura yake itakueleza mengi hata kama yeye ataamua asikuambie kwasababu zake zozote tu. Ally alisaidiwa na mtu ambaye hata walikua hawafahamiani na kuamua kumpa hifadhi katika sehemu ambayo yeye alikua anakaa. Pengine yeye alipofanya wala hakujua kama Ndugu Ally atakuja kuwa mmoja wa ma DJ HODARI na Hyper Man bora ambae nchi hii imewahi kuona.

    Leo ningependa tujifunze kuhusu hilo, kuhusu kuwa kind, kuhusu kuwapa watu nafasi kwenye maisha yetu na kutosubiri malipo kutoka kwao maana pengine yanaweza yasije lakini wewe tayari unakua ushamaliza kazi yako.

    Yangu matumaini story ya DJ Ally Bee itakua na impact kwenye maisha yako kama ambavyo imekua kwenye maisha yangu.

    Enjoy and stay BLESSED.

    Love,

    Salama.

    --- Support this podcast: https://podcasters.spotify.com/pod/show/yahstonetown/support
    Show more Show less
    1 hr and 5 mins

What listeners say about Salama Na

Average customer ratings
Overall
  • 5 out of 5 stars
  • 5 Stars
    1
  • 4 Stars
    0
  • 3 Stars
    0
  • 2 Stars
    0
  • 1 Stars
    0
Performance
  • 5 out of 5 stars
  • 5 Stars
    1
  • 4 Stars
    0
  • 3 Stars
    0
  • 2 Stars
    0
  • 1 Stars
    0
Story
  • 5 out of 5 stars
  • 5 Stars
    1
  • 4 Stars
    0
  • 3 Stars
    0
  • 2 Stars
    0
  • 1 Stars
    0

Reviews - Please select the tabs below to change the source of reviews.