Episodes

  • Eliot Berry, Mwingereza anayependelea kuishi Kenya| Kisa Changu Podcast
    Nov 27 2022
    Eliot Berry, Raia wa Uingereza alikuja Kenya akiwa na umri wa miaka 19 alipotumwa na mamaye kutembea. Anasema alikuwa msumbufu na mara nyingi alikuwa akitoroka shuleni lakini alipofika Kenya alihisi kuwa nyumbani na maisha yake yakabadilika. Alianza rasmi kuishi nchini Kenya mwaka 2011 na amejifunza Kiswahili na pia Sheng kwa lengo la kutangamana na watu wa matabaka yote. Aidha, kwenye mitandao ya kijamii anakojulikana kama Reverend Dad, amekuwa akiwafurahisha watu kwa video za ucheshi kutumia Kiswahili. Katika Kicha Changu Podcast wiki hii tunaangazia maisha ya Reverend Dad, katika mahojaino haya na Faith Kutere.
    Show more Show less
    15 mins
  • Familia zatafuta wapendwa wao, Mombasa | Kisa Changu Podcast
    Nov 6 2022
    Kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa familia mbili kwenye eneo la Likoni katika Kaunti ya Mombasa zinaendelea kuhangaika kuwatafuta wapendwa wao ambao wanaaminika kuchukuliwa kwa nguvu na maafisa wa Idara ya Usalama. Tumesema na familia ya Bakari Mwanyota mwenye umri wa miaka 38 wa Mtaa wa Consolata na familia ya Tunu Said mwenye umri wa miaka 55. Familia hizo mbili zinasema wapendwa wao walichukuliwa kwa nguvu mwezi Februari na Julai, 2021 na hadi sasa hawajui waliko. Robert Menza amezungumza na familia za wawili hao katika makala haya ya Kisa Changu Podcast.
    Show more Show less
    20 mins
  • Mlinzi wa Binafsi Aliyeponea Kifo | Kisa Changu Podcast
    Oct 29 2022
    Bernard Kibet amekuwa bawabu kwa zaidi ya miaka kumi. Japo kazi hii imemwezesha kuilisha familia yake na kuwasomesha watoto wake ni kazi ii hii ambayo imemsababishia machungu ambayo hatawahi kusahau kamwe. Kibet anasema wakati mmoja genge la majambazi lililokuwa kwenye eneo lake la kazi liliiba na kumpiga risasi kichwani bila kukusudia. Waliomwokoa walimchanganya na mili minane bila kukusudia tayari kupeleka katika hifadhi ya maiti lakini kwa bahati nzuri aliokolewa. Ilikuwa aje? Martin Ndiema amefanya mezungumzo na Kibet katika Podcast hii.
    Show more Show less
    12 mins
  • Kijiji Cha Walemavu, Bungoma | Kisa Changu Podcast
    Oct 15 2022
    Kijijini Namawanga, kilichoko eneo la Busunu Kaunti ya Bungoma kuna takriban familia 27 hivi. Kisicho cha kawaida ni kwamba katika kila familia kuna angalau mtoto mmoja mwenye ulemavu. Wapo waliozaliwa wakiwa na matatizo kuona, kuna wengine waliozaliwa bila viungo vya mwili kama vile miguu na mikono na wengine wanaugua ugonjwa wa seli-mundu yaani sickle cell. Duncan Waswa amefika katika kijiji hicho na kuzungumza na baadhi ya wakazi. Haya hapa masimulizi yao ya kuhuzunisha. Duncan Waswa amefika katika kijiji hicho na kuzungumza na baadhi ya wanakijiji. Haya hapa masimulizi yao ya kuvunja moyo.
    Show more Show less
    12 mins
  • Pesa za HELB ziliishia kampeni | Kisa Changu Podcast
    Sep 24 2022
    Stephen Kwisis, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Laikipia ana machungu baada ya kukosa kufaulu katika azma yake ya kuwa mbunge wakati wa uchaguzi mkuu wa Agosti 9, mwaka 2022. Kwisis mwenye umri wa miaka 24 anasema alitumia fedha za mkopo wa kufadhili elimu ya chuo kikuu, HELB kufanyia kampeni. Mwanasiasa huyo mchanga aliyekuwa akikabiliana na washindani 13 alipata kura 156 pekee. Amezungumza na Duncan Waswa kuhusu masaibu yanayomkumba katika masimulizi yafuatayo.
    Show more Show less
    7 mins
  • Kisa Changu Podcast: Mahangaiko ya wanasiasa wanawake wenye ulemavu; Sehemu ya 1
    Aug 4 2022
    Mwakilishi wa Kike wa Kaunti ya Machakos Rose Museo ana ulemavu. Museo aliyepata ulamavu huo ulemavu kufuatia ajali mwaka 2007 anasema changamoto hiyo haikumzuia kufanikisha ndoto yake ya kuwa kiongozi. Rose Mukonyo amezungumza naye anafafanua zaidi huku akiwashauri wanawake wengine wenye ulemavu kwamba wanaweza.
    Show more Show less
    25 mins
  • Wanawake walemavu siasani; Rose Museo | Kisa Changu Podcast Sehemu ya 1
    Jul 31 2022
    Mwakilishi wa Kike wa Kaunti ya Machakos, Rose Museo ni mwenye ulemavu. Museo aliyepata ulamavu huo ulemavu kufuatia ajali mwaka 2007 anasema changamoto hiyo haikumzuia kufanikisha ndoto yake ya kuwa kiongozi. Katika mazungumzo na mwanahabari wetu, Rose Mukonyo anawashauri wanawake wengine wenye ulemavu kwamba wanaweza kuafikia malengo maishani.
    Show more Show less
    25 mins
  • Kisa Changu Podcast: Uraibu wa mihadarati ulizamisha ndoto zangu maishani
    Jul 23 2022
    Silas Githaiga, mkazi wa Kijii cha Giciria, Kaunti ya Nyeri alikuwa mraibu wa mihadarati kwa miaka takriban 14. Anasema uraibu huo ulilemaza masomo yake na akiwa katika shule ya upili alisomea shule nne tofauti kwa vile alikuwa akifukuzwa kutokana na utovu wa nidhamu. Anasema tatizo hilo liliathiri ndoa yake likazima ndoto ya kuwa mhadhiri wa chuo kikuu na hata safari yake ya kwenda ughaibuni. Hata hivyo aliamua kurekebisha na hapo ndipo alipojiunga na chuo cha urekebishaji tabia. Kwa sasa maisha yake yamebadilika na ameamua kuwa mstari wa mbele kuwahamasisha vijana dhidi ya utumiaji wa dawa za kulevya vilevile kuwapa ushauri nasaha. Pata masimulizi kamili katika Kisa Changu Podcast na Edwin Mbugua.
    Show more Show less
    17 mins