Episodios

  • The Founders with Kennedy's Confessions - "Mchaka Mchaka"
    May 16 2023
    Meet a young entrepreneur Kennedy Mmari sharing his journey as a businessman.

    Hosted on Acast. See acast.com/privacy for more information.

    Más Menos
    52 m
  • The Founders with Ashura's Confessions - "Gigi".
    Nov 1 2022

    Dunia ya kidigitali ndio dunia ya sasa, kila kitu kina athiriwa moja kwa moja na teknolojia, tunaposema kila kitu tunamaanisha mpaka kwenye kazi na ajira. Tunakutana na Ashura ambae ni mmja wa waanzilishi wa jukwaa la wafanyakazi huru linalofahamika kama Gigspace.


    Ashura anatueleza mengi kuhusu wazo lake la kutoka kua mfanyakazi huru, mpaka kuunda jukwaa lake la wafanya kazi huru (Freelancers), kuna mengi ya kujifunza kutoka kwake.


    The Founders with Ashura's Confessions - "Gigi"


    Cheers!


    Hosted on Acast. See acast.com/privacy for more information.

    Más Menos
    51 m
  • The Founders with Lucas' Confessions - "Mali Shamba".
    Jul 27 2022

    Kama umewahi kusikia ile methali inayosema "Ukitaka mali utaipata shambani" basi kuna watu wanaweza kukuelezea maana yake vizuri zaidi. Mfahamu Lucas Malembo ambae ni CEO wa Malembo Farm. Ametufahamisha mengi sana kuhusu kilimo biashara, mtazamo wa wengi kuhusu biashara kupitia kilimo ni hasi, wengi hudhani kua sio rahisi kufanikiwa au ni kazi ya waliochoka kimaisha, Je ni kweli?.


    Lucas anatuaminisha wazi kabisa anatamani wengi, hasa vijana kujitokeza katika fursa za kilimo, maana kuna pesa na utajiri mkubwa. Kuna mengi sana ya kujifunza kutoka kwake, kwanzia mwanzo wa safari yake, hapa alipo na anapoelekea. Unatamani kutengeneza pesa kupitia kilimo? Maswali yako mengi Lucas amekupa majibu yake!. Enjoy and Learn.


    The Founders with Lucas' Confessions - "Mali Shamba"


    Cheers!


    Hosted on Acast. See acast.com/privacy for more information.

    Más Menos
    1 h y 15 m
  • The Founders with Muddy's Confessions - "Udambu-Udambu wa Muddy".
    Jul 11 2022

    Katika kila jambo kunahitaji nguvu kubwa kufika kule ambako unapotaka. Mfahamu Muddy Mabiriani, mtanzania alieacha ajira na kuamua kujishughulisha na uuzaji wa chakula akiwa mbobevu wa "Biriani". Ndoto zake na mitazamo yake kuhusu biashara anayofanya kwa ujumla vinafanya awe jinsi alivyo na ndivyo vimemfikisha hapa alipo mpka sasa.


    Kuna story nyingi sana unaweza kua unazisikia kuhusu yeye na biashara yake lakini waswahili wanasema "Ukitaka kujua utamu wa ngoma basi ingia uicheze". Tukakaa na muddy kupiga nae story kuhusu biashara yake, mwanzo wake alipo na anapotaka kufika. Kuna mengi sana unaweza kujifunza kwake, unaweza ukatafakari katika safari yako ya kuanzisha kile ambacho una kitaka either ni biashara au kampuni, ni wapi upite na wapi usipite. Karibu ujifunze kutoka kwa Muddy!


    The Founders with Muddy's Confessions - "Udambu Udambu wa Muddy"


    Cheers!


    Hosted on Acast. See acast.com/privacy for more information.

    Más Menos
    53 m
  • The Founders with Anna's Confessions - "Mtaji".
    Jun 16 2022

    As a fresh 2019 graduate, She sees an opportunity in fashion and design specifically nail products. Get to know alipita wapi? na alikutana na nini? mpka kufikia hapa alipo?. Challenges zipo but there's a saying "Dreams are worth more than money". Was it the same kwake?


    ANNA ROBERT is the brain behind ROBIANNAH Nail Products. Anna anapenda urembo aliamini tunahitaji brand yake!. Beauty is an art. She appreciates beauty and good-looking. She is certain that every woman does too. Moreover, it is a business; there is money to be made.


    The Founders with Anna's Confessions - "Mtaji"


    Cheers!


    Hosted on Acast. See acast.com/privacy for more information.

    Más Menos
    44 m
  • The Founders with Gerald's Confessions - "Bluetick za Uso".
    May 16 2022

    Kwenye maisha kuna watu ambao ukikutana nao, unaamini wana kitu kizuri ndani yao na bila ya shaka watakua na mafanikio mengi huko mbeleni. 


    Hii ni hisia ambayo mimi nimekua nayo toka siku ya kwanza naonana na Gerald. Ni kijana mwenye ndoto kubwa sana ambae anajitaidi kukimbizana na tecknolojia ya sasa. 


    Gerald Revocatus ni mwanzilishi wa kampuni ya VIJANATECH! Ni timu ya wataalam wenye vipaji vya IT wanaounganisha ujuzi, sanaa na hadithi za kibinafsi za kuvutia ili kuleta mageuzi ya kidigitali nchini Tanzania. 


    VIJANATECH pia wanaangalia matatizo yanayojitokeza sana katika jamii yetu na kuyatatua katika mtazamo wa Ki-teknolojia.


    Yangu matumaini uta-enjoy maongezi haya na utaokota mawili matatu pia ambayo yatakusaidia wewe kwenye maisha yako kama mwanzilishi, ili mambo yazidi kuwa mswano.


    "The Founders Confessions" - Bluetick Za Uso.


    Cheers 🥂


    Hosted on Acast. See acast.com/privacy for more information.

    Más Menos
    26 m
  • The Founders with Edgar's Confessions - "Vibes and Inshallah".
    Apr 27 2022

    Kutana na Edgar Mwampinge ambae ni Mwanzilishi wa kampuni inayofahamika kama WorkNasi pamoja na HEPHA. Kuna mengi ya kujifunza kutoka kwake, kutoka kua muhitimu wa shahada ya sheria mpaka kua mwanzilishi wa kampuni za teknolojia.


    Changamoto zipo na zinabadilika kadiri unavyoendelea kukua. Lakini kuna changamoto chache mwanzoni unapokua mwanzilishi. Na hizi chache ndio hufahamika zaidi.


    1. Namna ya kuanza hasa katika yale ambayo huna utashi nayo au elimu.
    2. Uchumi ni changamoto ambayo haikwepeki kwa wengi.
    3. Mazingira rafiki pia hua ni changamoto, kutokana na aina ya kampuni/biashara.


    Lakini katika yote haya Edgar bado anatuaminisha kwamba bado inawezekana kuanzisha kampuni/biashara yako. Kama yeye alifanikiwa basi na wewe unaweza kufanikiwa.


    The Founders Confessions - "Vibes and Inshallah"


    Cheers!


    Hosted on Acast. See acast.com/privacy for more information.

    Más Menos
    37 m
  • The Founders Confessions (The Introduction)
    Mar 5 2022
    Welcome to our Podcast series where we talk all about the journeys of many Top Notch People who created their Businesses and Companies from Scratch to Stardom.

    Hosted on Acast. See acast.com/privacy for more information.

    Más Menos
    1 m