Episodes

  • Sitaubadili uraia: Angela Okutoyi | Gumzo na Mwanaspoti Podcast
    Nov 27 2022
    Bingwa wa tenisi kwa wachezaji chipukizi chini ya miaka kumi na minane, Angela Okutoyi anasema hawaii kubadili uraia. Katika mazungumzo na Ali Hassan Kauleni, Okutoyi amesema wazi kwamba licha ya kupata nafasi ya kufanya hivyo ataendelea kuwakilisha Kenya katika mashindano ya tenesi.
    Show more Show less
    18 mins
  • Chakula bado ni cha Vibandani: Angela Okutoyi | Gumzo na Mwanaspoti Podcast
    Nov 14 2022
    Licha ya kutamba katika mashindano ya tenisi, Angela Okutoyi bado anapitia maisha magumu. Katika mahojiano na Mhariri wa Michezo, Ali Hassan Kauleni, mshindi huyo wa taji la Wimbledon anasimulia masaibu ambayo amepitia katika safari yake ya mchezo wa tenisi. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka kumi na minane anasema bado analazimika kukula vibandani licha ya ahadi kutoka kwa maafisa wa serikali ya kumsaidia.
    Show more Show less
    26 mins
  • Nilitengwa Ethiopia; Silvanus Otema | Gumzo na Mwanaspoti Podcast
    Oct 14 2022
    Aliyekuwa mchezaji wa timu ya kitaifa ya soka, Harambee Stars Silvanus Otema anasema alipitia wakati mgumu nchini Ethiopia baada ya kujiunga na klabu ya St. George. Otema anasema alitengwa na wachezaji wa klabu hiyo kutokana na uzuri wake. Pata uhondo kamili katika Podcast hii.
    Show more Show less
    15 mins
  • Gumzo na Mwanaspoti Potcast; Uzalendo au pesa!
    Jul 31 2022
    Wanariadha wenye asili ya Kenya wamekuwa wakikiwakilisha mataifa mbalimbali baada ya kubadili uraia. Merekani, Canada, Bahrain, Qatar, Israel ni miongoni mwa mataifa ambayo yamenufaika pakubwa kutoka kwa wanariadha waliozaliwa nchini Kenya. Mwanahabari wetu Walter Kinjo alizungumza na aliyekuwa Kocha wa timu ya taifa ya Riadha Mike Kosgei ambaye ameweka wazi sababu ambazo zimechangia wanariadha kubadili uraia.
    Show more Show less
    7 mins
  • Gumzo na Mwanaspoti Podcast; Magari ya hybrid ya safari rally hayauzwi
    Jul 4 2022
    Magari ya hybrid ambayo kwa mara ya kwanza yalitumika katika mashindano ya dunia ya uendeshaji magari hayauzwi ila yanatengezwa tu kwa ajili ya mashindano. Abdul Sidi ambaye alikuwa dereva vilevile msaidizi yaani navigator anasema magari ya hybrid yametengezwa na teknolojia ya juu zaidi na kwamba mtu wa kawaida haruhusiwi kuendesha. Sidi amezungumza na mwanahabari wetu, Walter Kinjo kuhusu teknolojia hii ya magari ya safari rally ya hybrid.
    Show more Show less
    8 mins
  • Gumzo na Mwanaspoti Podcast: Magari yetu ni ya viwango vya chini-Dennis Mwenda
    Jun 19 2022
    Dennis Mwenda ambaye ni dereva vilevile msaidizi katika mashindano ya Dunia ya Safari Rally anasema magari ambayo yanatumika na Wakenya katika mashindano ya Safari Rally ya WRC ni ya viwango vya chini. Katika mahojiano na mwanahabari wetu, Dennis anasema kutokana na ukosefu wa ufadhili ni vigumu sana kupata magari vya viwango vya juu kutokana na gharama. Dennis ambaye vilevile anaelezea safari yake katika uendeshaji magari ni miongoni mwa madereva ambao watashiriki mashindano ya Safari Rally makala ya mwaka 2022.
    Show more Show less
    10 mins
  • Gumzo na Mwanaspoti: Bado tuko kwenye ligi kuu ya FKF - Jakton Obure
    Jun 17 2022
    Afisa Mkuu Mtendaji wa Klabu ya Mathare United, Jakton Obure amesema watasalia kwenye ligi kuu ya FKF msimu ujao licha ya kushushwa daraja baada ya kukosa kushiriki mechi tatu mfululizo. Katika mahojiano na Ali Hassan Kauleni na Walter Kinjo, Obure anasema kwa mujibu wa sheria za FIFA ni kwamba kamati ya muda katika shirikisho la soka FKF haina uwezo wa kufanya maamuzi kuhusu ligi kuu ya soka FKF.
    Show more Show less
    8 mins
  • Gumzo na Mwanaspoti Podcast; Nina tajriba kuwa Rais wa FKF-Allan Wanga
    Jun 3 2022
    Allan Wanga anayewania kiti cha urais katika Shirikisho la soka la Kenya [FKF], alikuwa mchezaji wa timu ya Kitaifa ya Soka Harambee Stars. Wanga anaelezea mikakati aliyoweka katika kulenga kuwa Rais wa FKF. Katika mazungumzo na wanahabari wetu Ali Hassan Kauleni na Walter Kinjo, Wanga ambaye ni mfanyakazi katika Kaunti ya Kakamega anasema Kenya inahitajikiongozi ambaye ana ufahamu mkubwa wa masuala ya soka.
    Show more Show less
    8 mins